- Happiness

Furaha

Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. - Zaburi 5:11

Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele. - Zaburi 16:11

Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. - Zaburi 30:5

Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. - Zaburi 126:5

Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. - Psalms 128:1, 2

Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia. - Isaya 35:10

Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. - Yohana 15:11

Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu. - Warumi 14:17