Praise to God

Sifa njema kwa Mungu

Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. - Nehemia 8:10

Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. - Zaburi 34:1

Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. - Zaburi 50:23

Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya. - Zaburi 150

Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako. - Zaburi 89:15

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; - Zaburi 100:1, 2

Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. - Zaburi 92:1

Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi. - Zaburi 101:1

Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi. - Zaburi 97:1

Enyi wenye haki, mmfurahieni Bwana, Na kulishukuru jina lake takatifu. - Zaburi 97:12

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. - Zaburi 103:1, 2

Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. - Zaburi 149:1, 3-5

Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. - Zaburi 50:23

Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. - Matendo ya Mitume 16:25

Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. - 2 Mambo ya Nyakati 20:21,22

shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 19 Msimzimishe Roho; - 1 Wathesalonike 5:18

Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. - Waebrania 13:15

Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa. - Zaburi 71:8

Nami nitatumaini daima, Nitazidi kuongeza sifa zake zote. - Zaburi 71:14

Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa. - Zaburi 113:3

mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; - Waefeso 5:19, 20

Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. - Ufunuo wa Yohana 19:5