Can a Christian lose his salvation?


Je, Mkristo anaweza upoteza wokovu wake?

Kabla ya swali hili kujibiwa, neno "Mkristo" lazima lielezwe. "Mkristo" si mtu ambaye amesema maombi, au kutembea katikati mwa madhabahu, au wamelelewa katika familia ya Kikristo. Ingawa kila aina ya mambo haya inaweza kuwa sehemu ya maisha ya Mkristo, hayo sio mambo yale "hufanya" Kikristo. Mkristo ni mtu ambaye, kwa imani, amempokea na kumwamini kikamilifu Yesu Kristo kama mwokozi pekee (Yohana 3:16; Matendo 16:31; Waefeso 2:8-9).

Hivyo, pamoja na ufafanuzi huu katika akili, Mkristo anaweza kuupoteza wokovu? Labda njia nzuri ya kujibu swali hili muhimu sana ni kuchunguza ni nini Biblia inasema hutokea katika wokovu, na kujifunza ni nini kupoteza wokovu kunahuzisha. Hapa kuna mifano michache:

Mkristo ni kiumbe kipya. "Kwa hiyo, kama mtu ni katika Kristo, yeHata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya." (2 Wakorintho 5:17). Aya hii inazungumzia mtu kuwa kiumbe kipya kabisa kama matokeo ya kuwa "katika Kristo." Kwa Mkristo kupoteza wokovu, kiumbe kipya hufutiliwa na kuachwa.

Mkristo amekombolewa. "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo." (1 Petro 1:18-19). Neno "kukombolewa" inamaanisha ununuzi kufanyika, bei kulipwa. Kwa Mkristo kuupoteza wokovu, Mungu mwenyewe anaufutilia mbali ununuzi ambao aliulipia wa damu ya Yesu Kristo.

Mkristo amefanywa haki. "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu" (Warumi 5:1). Na "kuhalalisha" ina maana ya "kuwa waadilifu." Wale wote ambao humpokea Yesu kama Mwokozi ni "wametangazwa kuwa waadilifu" na Mungu. Kwa Mkristo kuupoteza wokovu, Mungu lazima alirudie maneno lake "asitanganze" kile ambacho hapo awali alikitangaza.

Mkristo ameahadiwa uzima wa milele. "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16). Uzima wa milele ni ahadi ya milele (milele yote) katika mbinguni pamoja na Mungu. Mungu anaahidi, "Amini na utakuwa na uzima wa milele." Kwa ameahadiwa kuishi milele, basi ni jinsi gani Mungu anaweza kuvunja ahadi hii kwa kuuchukua uzima wa milele?

Mkristo ameakikishiwa kutukuzwa. "Na wale aliwachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akwatukuza" (Warumi 8:30). Kama tulivyojifunza katika Warumi 5:1, kuhesabiwa haki hutangazwa wakati wa imani. Kwa mujibu wa Warumi 8:30, utukufu umehakikishiwa wale wote ambao Mungu amewafanya haki. Utukufu unahusu Mkristo kuupokea kamili ufufuo wa mwili wa mbinguni. Kama Mkristo anaweza kuupoteza wokovu, basi Warumi 8:30 ina makosa, kwa sababu Mungu hakuweza kuwahakikishia kutukuzwa wale wote ambao Yeye aliwachagua, waito, na kuwafanya haki.

Maelelezo zaidi ya kile hutokea katika wokovu inaweza kugawa. Hata hizi chache huiweka wazi zaidi kwamba Mkristo hawezi kuupoteza wokovu. Wengi, kama si zote, za kile Biblia inasema kinachotokea kwetu wakati sisi humpokea Yesu Kristo kama mwokozi itafutiliwa mbali kama wokovu utapotea. Wokovu hauwezi patilizwa. Mkristo hawezi kuwa si kiumbe kipya. Ukombozi hauwezi kutenguliwa. Uzima wa milele hauwezi kupotea na bado kuchukuliwa kuwa wa milele. Kama Mkristo anaweza kuupoteza wokovu, Mungu lazima alirudie neno lake na abadilishe mawazo yake- mambo akili- mbili mawilie maandiko yanatuambia kuwa kamwe Mungu hutenda.

Pingamizi zaidi la kila mara kwa imani kwamba Mkristo hawezi kuupoteza wokovu ni 1) Je! itakuaje kwa wale ambao tayari ni Wakristo na wanaendelea kuishi maisha yasiyo ya maadili? 2) Je! itakuaje kwa wale ambao tayari ni Wakristo na lakini baadaye wanaikanusha imani na kumkufuru Kristo? Tatizo la pingamizi hizi mbili ni kifungu katika “Wakristo ni akina nani.” Biblia inatangaza kwamba Mkristo wa kweli hawezi endelea kuishi maisha ya maadili mabaya (1 Yohana 3:6). Biblia inatangaza kwamba mtu yeyote ambaye anaiacha imani anaonyesha kwamba yeye kamwe hakuwa Mkristo (1 Yohana 2:19). Kwa hivyo, kati ya hizo pingamizi hakuna yenye ya halali. Wakristo hawawezi daima endelea kuishi maisha ya upotovu, wala wao kufuru na kumkana Kristo. Hatua hizo ni uthibitisho kwamba wao kamwe hawakukombolewa.

La! Mkristo, hawezi kuupoteza wokovu. Hakuna kitu kinachoweza kumtenganisha Mkristo na upendo wa Mungu (Warumi 8:38-39). Hakuna kitu kitakachomtoa Mkristo mikononi mwa Mungu ( Yohana 10:28-29 ). Mungu ako tayari na ana uwezo wa kuhakikisha na kudumisha wokovu Yeye ametupa. Yuda 24-25 ,

"Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina."




AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE