Ni nini maana ya ukombozi ya Kikristo ni nini?

Kila mtu anahitaji ukombozi. Hali yetu ya asili alikuwa na sifa ya hatia: "Kwa sababu wote wamefana dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Ukombozi wa Kristo ametuweka huru kutokana na hatia, kuwa "wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu" (Warumi 3:24).

Faida ya ukombozi ni pamoja na uzima wa milele (Ufunuo 5:9-10), msamaha wa dhambi (Waefeso 1:7), haki (Warumi 5:17), uhuru kutoka kwa sheria ya laana (Wagalatia 3:13), kupitishwa katika familia ya Mungu (Wagalatia 4:5 ), ukombozi kutoka katika utumwa wa dhambi (Tito 2:14; 1 Petro 1:14-18), amani na Mungu (Wakolosai 1:18-20), na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 6: 19-20). Kukombolewa, basi, ni kusamehewa, takazika, haki, kuwa huru, kuteuliwa, na kupatanishwa. Angalia pia Zaburi 130:7-8; Luka 2:38; na Matendo 20:28.

Neno kukomboa lamaanisha "kununua kutoka." Neno hilo lilitumika hasa katika kumbukumbu ya ununuzi wa uhuru wa mtumwa. Matumizi ya neno hili kwa kifo cha Kristo msalabani lasema wazi. Kama sisi "tumekombolewa," basi hali yetu mbeleni ilikuwa ya utumwa. Mungu amenunua uhuru wetu, na sisi hatuko tena katika utumwa wa dhambi au sharia ya Agano la Kale. Matumizi ya kiriwaya ya "ukombozi" ni mafundisho ya Wagalatia 3:13 na 4:5.

Kinachohusiana kwa kabiru na dhana ya Kikristo ya ukombozi ni neno fidia. Yesu alilipa gharama ili tutolewe katika dhambi na matokeo yake (Mathayo 20:28; 1 Timotheo 2:6). Kifo chake kilikuwa badala ya maisha yetu. Kwa kweli, maandiko yako wazi kabisa kwamba ukombozi unawezekana tu "kwa njia ya damu yake," yaani, kwa kifo chake (Wakolosai 1:14).

Mitaa ya mbinguni itajaa wafungwa wa zamani ambao, kwa njia ya sifa isiyo yao wenyewe, wanajikuta wamekombolewa, samehewa, na huru. Watumwa wa dhambi wamekuwa watakatiafu. Si ajabu tutakuwa na kuimba wimbo mpya - wimbo wa sifa kwa mkombozi huyo aliyeuawa (Ufunuo 5:9). Tulikuwa watumwa wa dhambi, tulihukumiwa utengano na Mungu wa milele. Yesu alilipa gharama ili atukomboe,hii ilisababisha uhuru wetu kutoka utumwa wa dhambi na wokovu wetu kutokana na matokeo ya milele ya dhambi hiyo.



AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE