Is eternal security Biblical?



Je, usalama wa milele ni kibiblia?

Watu wanapomjia Yesu kama mwokozi wana unganishwa katika ushirika na Mungu unaowahakikishia usalama wa milele. Yuda 24 inasema, "kwa yule anayeweza kuwalinda msije mkajikwaa na kuwawasilisha mbele za utukufu wake mkiwa bila mawaa yoyote mkijawa na furaha kuu." Nguvu ya Mungu inatosha kumfanya muumini asianguke dhambini. N i jukumu lake, sio letu kutuwasilisha mbele za utukufu wake tukiwa hatuna mawaa.usalama wetu wa milele ni kwa sababu ya Mungu kutuhifadhi si bidii zetu wenyewe.

Bwana Yesu kristo alisema, "nawapa uzima wa milele, nao hawatapotea; kwa kuwa hakuna anayeweza kuwatoa mikononi mwangu. Baba yangu, aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote; hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwa Baba yangu" (Yohana 10:28-29b). Baba na Mwana wametushikilia mikononi mwao. Ni nani awezaye kututoa mikononi mwa Baba na Mwana pamoja?

Waefeso 4:30 inatuambia waumini "wamehifadhiwa kwa ajili ya siku ya ukombozi." Kama waumini hawangekuwa na uasalama wa milele kuhifadhiwa kwao kungekuwa si kwa kudumu na kungeisha tu siku ile ya kufanya dhambi ama kutoamini. Yohana 3:15-16 inatuambia ya kwamba yeyote atakayemwamini Yesu kristo "atakuwa na uzima wa milele." Kama mtu angeahidiwa uzima wa milele halafu uondolewe kwake, basi haungekuwa wa milele kutoka mwanzoni. Kama uasalama wa milele haungekuwako basi uzima wa milele katika biblia pia ungekuwa na kasoro.

Mjadala unatokea katika warumi 8;38-39, "kwa kuwa nimeshawishika ya kwamba si kifo wala uzima, malaika wala pepo, muda wa sasa wala ujao wala mamlaka yoyote, urefu wala kina wala chochote kilichoumbwa kitatutenganisha na upendo wa Mungu uliomo ndani ya kristo yesu Bwana wetu." Usalama wetu wa milele umenunuliwa na kristo, umeahidiwa na Baba na umehifadhiwa na Roho mtakatifu.



AMAZING GRACE BIBLE INSTITUTE